TRA YAZINDUA MFUMO WA KUWASILISHA RITANI KIELEKTRONIKI
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dkt. Edwin P. Mhede (mwenye tai nyekundu) akiongea na Wajumbe wa Bodi, Menejimenti ya TRA pamoja na Waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kuwasilisha ritani za Kodi (e-filing) leo Jijini Arusha. Mkurugenzi wa Mifumo ya TEHAMA wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) (kushoto) akielezea namna Mfumo wa Kuwasilisha Ritani za Kodi unavyofanya kazi mbele ya Wajumbe wa Bodi, Menejimenti ya TRA pamoja na Waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kuwasilisha ritani za Kodi (e-filing) leo Jijini Arusha. Wajumbe wa Bodi, Menejimenti ya TRA pamoja na Waandishi wa habari wakifuatilia uzinduzi wa Mfumo wa Kuwasilisha ritani za Kodi (e-filing) leo Jijini Arusha. ……………………………………………………………….. Na Rachel Mkundai, Arusha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanzisha mfumo wa uwasilishaji wa ritani za kodi kwa njia ya kielektroniki (e-Filing System) ukiwa na lengo kurahisisha uwasilishaji wa ritani za kodi na kupunguza gharama kwa upand...