UN yamuunga mkono Magufuli kutokomeza ukatili wa mwanamke Ikungi
Picha ya pamoja ya Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi(mwenye kilemba) na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na wadau mbalimbali wa maendeleo mara baada ya uzinduzi wa mradi Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Rehema Nchimbi(kulia) akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania, Zlatan Milisic baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi Na John Mapepele, Ikungi MKUU wa Mkoa wa Singida Mhe, Dk. Rehema Nchimbi leo amezindua miongoni mwa miradi mikubwa iliyowahi kutekelezwa nchini, mradi wa pamoja baina ya Mashirika ya Kimataifa ya UN Women na UNFPA kupitia ufadhiri wa Shirika la KOICA wa Tuufikie usawa wa jinsia kupitia kuwawezesha wanawake na wasichana utakaogharimu takribani bilioni 11.5 za kitanzania ambao utatekelezwa katika Wilaya ya Ikung...