Posts

Showing posts from February, 2022

Mhe. Mchengerwa apongeza watanzania kuongoza Kili Marathon 2022

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewapongeza watanzania kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mbio za Kilimanjaro Marathon na kuongoza katika mbio hizo tofauti na miaka ya nyuma ambapo mataifa mengine yamekuwa yakiongoza. Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo leo, Februari 28, 2022 na kufafanua kuwa mwitikio huo mkubwa umetokana na kazi nzuri ambayo iliyofanywa na Rais wa  Samia Suluhu Hassan toka akiwa Makamu wa Rais ambapo aliongoza kuhamasisha riadha na kuanzishwa kwa klabu za mazoezi (jogging clubs) kwenye kila mkoa hapa nchini. Aidha amesema mikakati kabambe iliyowekwa na Serikali ya sasa kwenye Sekta ya michezo inakwenda kuleta mapinduzi makubwa ikiwa ni pamoja na kutoa ajira nyingi kwa wananchi. Katika mashindano hayo mtanzania Alyce Simbu aliongoza  kilomita 42  aliyetumia muda wa 02:16:30 wakati kwenye kilomita 21 nafasi ya kwanza hadi ya tatu zilichukuliwa na watanzania zikiongozwa na Emmanuel Ginniki (01:00:34), akifua...

MHE. GEKUL AELEZA MIKAKATI YA KUKUZA RIADHA KILI MARATHONI

Image
  Na. John Mapepele  Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Pauline Gekul amewapongeza waandaji wa mbio za Kilimanjaro Marathoni huku akifafanua kwamba tukio hilo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Michezo nchini  inayosisitiza ushiriki wa pamoja kati ya Serikali na wadau  katika kuendeleza michezo mbalimbali ikiwemo riadha.  Mhe. Gekul ameyasema hayo leo Februari 27, 2022 wakati akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) ili atoe hotuba yake kwenye kilele cha mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon, 2022 kwenye viwanja vya Chuo kikuu cha Ushirika Moshi.  “Sisi familia ya michezo tunajivunia uwepo wa tukio kubwa namna hii linalowaleta pamoja wanamichezo na wapenzi wa riadha kutoka katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi yetu, kipekee niwapongeze Kilimanjaro Premium Lager kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukuza michezo hapa nchini”. Amesema Mhe. Gek...

MHE. MCHENGERWA ATEMBELEA MAONESHO YA DUBAI EXPO

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa   ametembelea banda la Tanzania katika Maonesho ya EXPO Dubai 2020 yanayoendelea katika Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu na kupongeza  waoneshaji baada ya kujionea jinsi Tanzania inavyotumia   maonesho hayo ya Kitamaifa kujitangaza.  Mhe, Mchengerwa. jana Februari 24, 2022 amepita kukagua kwenye mabanda hayo ya maonesho na kuhimiza utoaji wa maelezo kiufasaha ili wageni wanaotembelea mabanda hayo  watambue vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana nchini hatimaye wafike kutembelea Tanzania. Katika mabanda hayo, Tanzania inajitangaza  kupitia fursa mbalimbali za Utalii, Madini, Nishati, Kilimo na Uwekezaji kwa wageni.  Mbali na maonesho ya kuonesha fursa mbalimbali pia Tanzania kwa mara ya kwanza imeutambulisha Utamaduni wa Tanzania kupitia muziki wa singeli duniani katika maonesho haya kupitia  mfalme wa singeli nchini Sholo Mwamba ambaye amewache...

MHE. MCHENGERWA ATAKA SINGELI IITEKE DUNIA DUBAI EXPO LEO

Image
  Na John Mapepele  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewataka wasanii wanaopanda leo Februari 24,2022 kuiwakilisha Tanzania kwenye Maonesho makubwa ya kimataifa ya Dubai Expo, Mfalme wa Singeli Sholo Mwamba na Mkongwe wa Muziki wa Asili wa Tanzania Mrisho Mpoto kuendelea kutoa burudani ya kukata na shoka ili kuitangaza Tanzania kimataifa.  Mhe. Mchengerwa amesema haya leo Februari 24,2022 wakati ambapo Sholo Mwamba anatarajia kuendelea kuwaipagawisha dunia kwa nyimbi za singeli  majira ya saa 11:00 jioni  kwenye ukumbi wa *Earth Stage* baada ya  kufanya  vizuri kwenye onesho lake  la awali Februari 22, 2022 na kuwaacha  umati uiliofika   kucheza naye huku wengine wakichukua picha kwa ajili ya matumizi yao. “Tunataka Singeli na muziki wa kwetu uiteke dunia ambapo kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeanza  vizuri safari ya mapinduzi makubwa  ya sanaa kwenye anga za kimataifa” amesisitiza Mhe. Mchenge...

MAMA NA MICHEZO

Image

SHOLO MWAMBA KUSIMAMISHA DUNIA DUBAI EXPRO LEO, KESHO

Image
  Na. John Mapepele Mfalme wa muziki wa Singeli nchini, Sholo Mwamba pamoja na msanii wa kizazi kipya Saraphina leo Februari 22, 2022 wanatarajia kupanda   na kuionyesha dunia miziki kutoka Tanzania kwenye onesho kubwa duniani la Dubai Expro.  Kwa mujibu wa ratiba ya waandaji wa onesho hilo Sholo  Mwamba  ndiye anayeanza kupanda  majira ya saa 9:30 alasiri  na Saraphina anapanda  majira ya saa 10:30 jioni ambapo wote watapanda kwenye ukumbi wa Sea Stage. Akizungumza kutoka Dubai, muda mfupi kabla ya kupanda jukwaani Sholo Mwamba amesema atahakikisha kupitia shoo ambazo anazozifanya, Singeli inakwenda kuwepo kwenye sura ya dunia. Ameongeza kuwa muziki wa Singeli una nafasi kubwa ya kuitambulisha Tanzania na kuvutia watalii wengi kuja kutembelea, hivyo atahakikisha wageni watakaohudhuria onesho hilo wanavutiwa  na muziki huo.  Sholo amepangiwa kutumbuiza mara tatu kwenye onesho hilo leo, kesho Februari 23, majira ya saa 10: 30 jioni w...

Mhe. Mchengerwa awaalika wananchi Tamasha la Serengeti

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa wito kwa wananchi wote kushiriki kwenye tamasha kubwa Tanzania na Afrika la Muziki la Serengeti (Serengeti Music Festival) litakalofanyika Machi 12, 2022 jijini Dodoma ili kujionea hazina ya vipaji vya wasanii nchini. Mhe. Mchengerwa amesema haya, hivi karibuni jijini Dar es Salaam ambapo amefafanua kuwa tamasha hili ndiyo tamasha kubwa linaloratibiwa na Serikali likiwa na lengo la kuibua vipaji vya wasanii pia kutangaza vivutio vilivyopo nchini ili kuliingizia taifa mapato kutokana na hazina ya utalii uliopo.  Aidha, amesema tamasha hilo litahusisha wasanii zaidi ya hamsini wa miziki ya aina mbalimbali ambao watatumbuiza   ili kuleta vionjo na radha tofauti tofauti.  “Tamasha hili linaleta muunganiko wa kipekee kabisa linaloonyesha tasnia ya burudani na utalii na ndiyo maana tumetumia jina la Mbuga yetu bora Afrika na duniani ya Serengeti ili kuwavutia wageni kutoka sehemu m...

MAELEKEZO YA MHE. MCHENGERWA YAFIKIA PAZURI

Image
  Na. John Mapepele  Maelekezo ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ya kutaka mchakato wa mwaka huu wa utoaji wa Tuzo za Muziki  bila upendeleo  yamefika  mahali pazuri. Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Matiko Mniko, leo Februari 21, 2022 imeeleza kuwa jumla ya kazi 402 zimewasilishwa kuanzia Februari 9, 2022 baada ya zoezi la kuwaelimisha wadau kukamilika na kuwa BASATA limeamua kuongeza muda wa siku saba ili kutoa nafasi kwa wasanii wengi kushiriki. “Tunaongeza siku 7 kwa ajili ya wasanii kuwasilisha kazi katika vipengele vya Tuzo za Muziki Tanzania (TMA 2021)” imefafanua taarifa hiyo.  Pia taarifa hiyo imefafanua kwamba mwisho wa kuwasilisha kazi hizo ni Machi mosi mwaka huu kupitia link www. tanzaniamusicawards.info  Akizungumza kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Utoaji wa Tuzo za Muziki na Ugawaji wa Mirahaba kwa Wasanii Januari 28, 2022 kwenye Ukumbi wa kimataifa wa Julius Nye...
Image
  Na. John Mapepele Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Pauline Gekul amezitaka Halmashauri zote nchini kuhamasisha programu ya kufanya mazoezi kuanzia ngazi ya mtaa ili kuimarisha afya kwa jamii na kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan za kuibua vipaji vya michezo kuanzia ngazi ya chini. Mhe. Gekul amesema hayo leo Februari 20, 2022, alipokua Mgeni Rasmi kwenye kilele cha Bonanza kubwa lililoandaliwa na Umoja wa Vilabu vya jogging klabu Mbagala, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza mbio za takribani kilomita 7.5 kuanzia Mbagala hadi Mtoni Kijichi. Amezitaka Klabu za Mazoezi kote nchini kuhakikisha zinashirikisha kikamilifu makundi maalum ya jamii kwenye siku za mazoezi, huku akitoa pongeza kwa umoja wa Mbagala Jogging Klabu kwa kuandaa tamasha hilo ambalo amelielezea kuwa limekuwa la mafanikio makubwa. Aidha, ametoa wito kwa wananchi wote kutenga muda kila siku kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao. “Akina mama wenzangu ujanja ...

MOROCCO YAKUBALI KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KWENYE MICHEZO

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Februari 15, 2022 amekutana na Balozi wa Morocco nchini Mhe. Zakaria Elgoumiri na kufanya mazungumzo ya kuendeleza sekta za michezo, utamaduni na Sanaa ambapo  Balozi amesisitiza serikali yake ipo tayari kushirikiana na Tanzania kwa faida ya wananchi wa nchi hizo. Mhe. Mchengerwa amesema Serikali ya Tanzania na Morocco zimekuwa na uhusiano mzuri katika sekta  hizo  toka  muda mrefu  hali ambayo  imewafanya  viongozi wakuu wa nchi zote  kufanya ziara na  kubadilishana  uzoefu  wa sekta hizo. Akiwa katika kikao hicho ambacho aliambatana na Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi, Mkurugenzi wa michezo nchini Yusufu Singo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Michezo (BMT) Neema Msitha wamekubalina  na ujumbe wa Mhe. Balozi wa kuendelea kushirikiana  kwenye sekta  hizo.  Ameyataja  baadhi ya maen...

MCHENGERWA AIPONGEZA WASAFI KWA KUKUZA VIPAJI VYA WASANII

Image
  John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameipongeza Kampuni ya Wasafi kwa kukuza sanaa ya muziki na kuzalisha ajira kwa vijana wengi hapa nchini. Akizungumza kwenye hafla ya Usiku wa Mahaba Ndi Ndi Ndi siku ya wapendanao Februari 14, 2022 jijini Dar es Salaam amesema Wasafi ina mchango mkubwa katika kuibua na kukuza vipaji vya wanamuziki. " Naomba nikuhakikishie Serikali ipo pamoja na nyie katika kukuza sanaa " amesema Mhe.Mchengerwa Aidha, amesema Serikali inakwenda kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Wasafi mtaa kwa mtaa, kijiji kwa kijiji hadi mkoa kwa mkoa kutafuta vipaji vya wasanii lengo ni kuwashindanisha na kuwaendeleza. Ameongeza kuwa, wizara inakwenda kuendeleza mapinduzi ya ukuzaji wa Sanaa ili kutoa ajira zaidi kwa vijana katika ngazi ya kitaifa na kimataifa. Amefafanua kwamba kufanya hivyo ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ya kutaka kuboresha sekta hiyo ili wasanii nchini waweze kunufaika na kazi zao. Kwa upande...
Image
        *************** Na. John Mapepele Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi amepamba hafla ya Usiku wa Mahaba ndi ndi ndi baada ya kuandaliwa keki maalum ya siku yake ya kuzaliwa na kuimbiwa wimbo wa kuzaliwa ulioongozwa na Diamond Platnumz. Dkt. Abbasi alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa waliokuja kushiriki kwenye hafla hiyo tarehe 14 Februari 2022 ambayo ni siku ya wapendanao (Valentine) na ghafla mshereheshaji wa hafla hiyo Zembwela kutangaza kuwa wasafi wameandaa keki maalum kwa Dkt Abbasi. Kwa upande wake Dkt. Abbasi aliishukuru Wasafi kwa kitendo hicho cha kumpa keki na kumwimbia wimbo wa kuzaliwa. " Ndugu zangu niseme wazi kuwa sikutegemea wala kuwaza hii surprise, ninawashukuru sana, kitendo mlichonifanyia hakiwezi kunitoka kwenye kumbukumbu za maisha yangu." Alisisitiza Dkt. Abbasi. Katika hafla hiyo wasanii mbalimbali walitumbuiza huku msanii maalum wa siku Zuchu akikonga nyoyo za washabiki huku mamake bi Hadija Kopa na Bosi wa...

Waziri Mchengerwa atoa maelekezo mazito ya kuboresha soka nchini

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa leo Februari 14, 2022 ametoa maelekezo mazito kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) yanayolenga kuboresha mchezo wa mpira wa miguu nchini. Maelekezo hayo ameyatoa katika mkutano wa Waandishi wa Habari aliofanya katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Februari 14 baada ya kufanya kikao na Viongozi wa TFF, BMT na watendaji wa Wizara. Amefafanua kuwa Serikali ipo katika mikakati kabambe ya kuboresha miundombinu ya michezo katika shule 56 nchini ikiwa ni pamoja na kufunga mashine za kisasa za kufuatilia michezo (VAR) kwenye  viwanja vitano  kwa kuanzia pamoja na kujenga  vituo  vikubwa vya michezo. Akitoa  maelekezo ya Serikali,  Mhe. Mchengerwa amesema BMT likutane na TFF mara moja kujadili namna ya  kudhibiti vitendo  vya  ukiukwaji wa Sheria na taratibu za mchezo huo pendwa nchini ambapo pia ames...

Mhe. Mchengerwa apongeza ubunifu wa wadau wa tamasha la Sauti za Busara

Image
  Na. John Mapepele  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amewapongeza  wadau mbalimbali wa Sanaa walioshiriki kwenye tamasha la Sauti za Busara Zanzibar kwa ubunifu wao na  kuwataka waendelee kutumia  matamasha hayo kutangaza  bidhaa na huduma wanazozitoa. Mhe. Mchengerwa  ametoa wito huo alipotembelea   mabanda yaliyokuwa yakionesha bidhaa na huduma zao kwenye kilele cha Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Februari 13, 2022. Mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotions, Mhe. Simai Mohamed Said ambao ndiyo waandaaji wa tamasha hilo amemshukuru Mhe. Mchengerwa kwa kutembelea wadau wa  tamasha hilo huku akisisitiza kuwa  kitendo hicho kimeonesha anathamini mchango wa wadau hao. Mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotion, Sinai Mohamed Said  akimtambulisha Mhe. Mchengerwa kwa mmoja wa wadau kwenye banda la Benki ya CRDB Mhe. Mchengerwa akiwa na kikosi cha mfalme wa Singeli nchini Sholo Mwamba kabla ya kikosi kupan...

Mhe. Mchengerwa aikaribisha dunia Tamasha la Serengeti kupitia Sauti za Busara

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amewakaribisha  wageni mbalimbali waliohudhuria tamasha  kubwa  la kimataifa la Sauti za Busara  kutoka  sehemu  mbalimbali duniani kushiriki kwenye  tamasha la kihistoria  la muziki la Serengeti litakali fikia kilele chake Machi 12, mwaka  huu jijini Dodoma. Akizungumza kwenye kilele  cha Tamasha la Sauti za Busara usiku wa kuamkia leo  Februari 14, 2022 huko zanzibar amesema  Serikali inakwenda  kuandaa matamasha makubwa  ya kihistoria ambayo yataonesha  utamaduni wa  kitanzania, hivyo dunia inakaribishwa kushuhudia tukio hili la kihistoria na kimataifa. "Naomba kutumia nafasi hii  kuwakaribisha  kwenye  Tamasha la Serengeti na Tamasha la kimataifa la Sanaa na Utamaduni  la Bagamoyo ambayo yanakwenda  kuionyesha dunia  utajiri wa utamaduni  na vivutio vya utalii duniani". Ameongeza Mhe....