Waziri Mchengerwa atoa siku 30 kwa BMT kutengeneza mifumo ya kusajili ya kielektoniki
Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amelielekeza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuhakiksha ndani ya mwezi mmoja linatengeneza mfumo wa kieletroniki wa kusajili vyama vya michezo ili kuondoa usumbufu kwa wadau unaojitokeza. Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo Oktoba 27, 2022 wakati akizindua program ya “Mpira Fursa” inayoratibiwa na Taasisi ya Karibu Tanzania (KTO) na kugawa vifaa vya michezo kwa Vyuo vya Wananchi vya Maendeleo 54 kote nchini na shule za msingi 86. Ameutaka uongozo wa shule ambazo zitabahatika kupata vifaa vya soka, kuwaruhusu wasichana kucheza soka na kuvitumia vifaa hivyo kwa uangalifu na kwa madhumuni yaliyokusudiwa. Ameipongeza KTO kwa kuanzisha program hiyo ya kupeleka michezo katika vyuo vya wananchi vya maendeleo na shule za msingi huku akifafanua kuwa huo ni utekelezaji wa maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanza...