BARAZA LA WAFANYAKAZI LATAKIWA KISIMAMIA UTENDAJI KAZI, NIDHAMU
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa, amewataka wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kuhakikisha kuwa wanasimamia ipasavyo utendaji kazi pamoja na nidhamu ya watumishi ili kuongeza ufanisi wa Taasisi. Bw. Nyaisa ametoa agizo hilo leo tarehe 11 Novemba, 2022 wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi kinachofanyika mkoani Morogoro. Bw. Nyaisa amesema kwakuwa Baraza la Wafanyakazi ni chombo cha ushirikishaji wa watumishi na linaundwa na wajumbe kutoka Menejimenti ya BRELA, viongozi wa Chama cha Wafanyakazi (TUGHE) na wawakilishi wa watumishi kutoka idara mbalimbali, wajumbe wote wanao wajibu wa kusimamia utendaji kazi pamoja na nidhamu ya watumishi ili kutoharibu taswira ya Taasisi. Bw. Nyaisa amesema pia viongozi wa TUGHE kama wajumbe wa Baraza wanapaswa kufuatilia maslahi ya wafanyakazi kwa kushirikiana na Menejimenti, hivyo wanapoona ...