RAIS SAMIA MGENI RASMI KATIKA ZOEZI LA UFUNGUZI BWAWA LA MWALIMU NYERERE DESEMBA 22,2022
Waziri wa Nishati Januari Makamba(wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la kuanza kujaza maji katika bwawa la Julius Nyerere(JNHPP) lililopo Rufiji mkoani Pwani.Tukio hilo la kuanza kujaza maji linatarajiwa kufanyika Desemba 22 mwaka huu ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.Kulia kwenye picha hiyo ni Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Maharage Chande na kushoto ni viongozi kutoka Wizara ya Nishati. Baadhi ya wakandarasi wa ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere wakiwa kwenye kikao cha Waziri wa Nishati Januari Makamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kujazwa maji kwa bwawa hilo tukio ambalo litafanyika Desemba 22 mwaka huu. Muonekano wa handaki la kuchepusha maji kama ambavyo linaonekana baada ya ujenzi wake kufikia asilimia 78.68. Waziri wa Nishati Januari Makamba akijadiliana jambo na maofisa wa TANESCO pamoja na Wizara ya Nishati leo Desemba 18 mwaka 2022 baada ya...