Royal Tour imeleta mazao lukuki ya utalii- DK Abbasi
Na John Mapepele Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii na Mwenyekiti wa Kamati ya Kuitaingaza Tanzania ya Royal Tour, Dkt. Hassan Abbasi amesema wakati Tanzania imetimiza mwaka mmoja toka Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan atoke ofisini na kucheza filamu ya Royal Tour, kumezaliwa mazao mbalimbali ya utalii hapa nchini. Dkt. Abbasi ametoa kauli hiyo leo Mei 1, 2023 wakati akihitimisha mjadala wa kitaifa kwenye mtandao (Zoom Meeting) uliojumuisha wadau mbalimbali wa utalii duniani na kurushwa mubashara ya mitandao na vyombo mbalimbali vya habari ulioangazia mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja wa Royal Tour. Amesema kutokana shuhuda nyingi zilizotolewa na wadau kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa katika kipindi kifupi tangu Roal Tour ilipozinduliwa inapaswa kila mtanzania kuwa balozi wa kuitangaza Tanzania ikiwa ni mkakati wa kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu...