Mhe. Mchengerwa ahesabiwa, asisitiza watu wote kuhesabiwa

 



Na John Mapepele, Rufiji .


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa wito kwa wanamichezo na wasanii wote kujitokeza kuhesabiwa  ili Serikali iweze  kupanga mipango ya maendeleo.

Akiongea mara baada ya kuhesabiwa leo, Agosti 23, 2022 kwenye makazi yake Ikwiriri - Rufiji  amesema mafanikio ya kizazi cha kesho yatatokana na kujua idadi sahihi ya takwimu  za sasa.

"Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa zoezi hili la sensa kwa kuwa  linalokwenda kutusaidia sana kuleta maendeleo" ameingeza Mhe. Mchengerwa


Aidha, amesema sensa  ya mwaka huu ni muhimu  katika sekta za michezo, na sanaa kwa kuwa itasaidia  kupanga namna bora ya kuwahudumia watanzania kwenye sekta hizo.

Amesema hiyo itasaidia kupanga namna na kujenga miundombinu  ya michezo kama vile viwanja vya michezo na  arena  za michezo.

Amefafanua kuwa sensa itasaidia  mipango ya kibajeti kuandaa kanzi data ya michezo na kutafuta vipaji vya wasanii na michezo.

Amesema kutokana na umuhimu wa zoezi hili Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo iliamua  kuja na kampeni maalum ya SENSABIKA ya kuhamasisha watu  wote kuhesabiwa.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi wa jimbo la Rufiji na watanzania wote kujitokeza kuhesabiwa.

Comments