Tanzania na Falme za Kiarabu waja na tamasha kubwa la Utamaduni

 

Na John Mapepele

Tanzania kwa kushirikiana na  nchi zote za falme za kiarabu inatarajia kufanya  tamasha kubwa la Utamaduni Februari mwakani jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na leo Agosti 18, 2022 na  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa baada ya kumaliza mazungumzo na Balozi wa Qatar nchi, Mhe. Husain Ahmad Al- Homaid aliyeambatana na ujumbe kutoka nchini Kuwait.

Aidha, amefafanua kuwa nchi hizo kabla ya uamuzi huo walitafiti na kuona kuwa  Tanzania imebarikiwa kuwa na Utamaduni tofauti na nchi nyingi duniani, hivyo kufanya tamasha hilo la pamoja litakuwa na faida kubwa kwa pande zote mbili.

Amesema maonesho  hayo ni maalum ya kiutamaduni ambapo yatajikita katika Sanaa za uchoraji, uchongaji pamoja na nyimbo.


Ameongeza kuwa Utamaduni na sanaa za Tanzania zina historia ndefu katika ukombozi wa Bara la Afrika ambapo amesisitiza kuwa Baba wa taifa wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere aliwaunganisha watanzania hadi kupata uhuru kwa  nyimbo, uchoraji na uchongaji wa vinyago.

Naye Mhe Balozi Al- Homaid amesema kundi la wasanii linalotarajia kuja Tanzania ni la wasanii wa kike likijumuisha wasanii wachache wa kiume.

Ameishukuru Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais. Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano mkubwa katika sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo.


Comments