Mhe. Mchengerwa awakabidhi Bendera Taifa Queens, awataka wafuzu Kombe la Dunia.

Na John Mapepele
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewakabidhi Bendera yaTaifa timu ya Taifa ya Netiboli ya Taifa Queens kama ishara ya kuwaaga kwenda kwenye mashindano ya kufuzu kushiriki Kombe la dunia yanayofanyika nchini Afrika Kusini.
Akikabidhi bendera hiyo leo Agosti 18, 2022 jijini Dar es Salaam, Mhe. Mchengerwa amewataka kutanguliza uzalendo na utaifa katika mashindano hayo ili kufanya vizuri na hatimaye kufuzu kuingia kwenye mashindano ya dunia.
“Naomba niwaambie ndugu zangu nnyie mnaweza kabisa kuandika historia ya kuwa timu ya tano katika nchi yetu kuingia kwenye mashindano ya dunia endapo mtakuwa wazalendo, nendeni mkacheze kufa na kupona kama ni kuvunjika mkavunjikie uwanjani lakini mrudi na ushindi nyumbani, nasi tutawapokea kwa heshima kubwa” Amefafanua Mhe. Mchengerwa.
Aidha, amewataka watambue kuwa wakifanya vizuri watakuwa wamefungua ukurasa mpya wa maisha yao kwa kuwa timu kubwa duniani zitawanunua kitu ambacho kitawafanya wabalishe maisha yao kwa ujumla.
Pia amesema kwa sasa dhamira ya Serikali ni kuendelea kusaidia michezo yote hususa ile inayofanya vizuri ili timu hizo zifike mbali zaidi.
Kwa upande mwingine amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa jitihada zake kubwa anazozifanya kuinua michezo nchini


Comments
Post a Comment