Posts

Showing posts from September, 2022

RAIS SAMIA AWAPA SALAMU TEMBO WARRIORS, MHE. MCHENGERWA ATOA AHADI NONO WAKISHINDA

Image
  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anaipongeza  Timu ya Taifa ya Tembo Warriors kwa kufuzu kombe la Dunia kwa watu wenye ulemavu linalotarajiwa kufunguliwa Septemba 30, 2022 na kuitaka kutanguliza uzalendo na kujituma ili warudi na Kombe nyumbani. Akizungumza kwa njia ya simu kupitia kwa Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi Waziri Mchengerwa amesema Serikali ya Tanzania ipo pamoja na wao katika kila hatua na ndio maana Rais ameridhia viongozi wa Wizara kuambatana nao katika fainali hizo. “Rais na Serikali yenu ipo pamoja na nyinyi, nendeni mkalipiganie Taifa, onesheni uzalendo na kuhakikisha mnarudi na Kimbe nchini na hiyo itakuwa ni zawadi kwake Mhe. Rais na Tanzania kwa ujumla”’ amefafanua Mhe. Mchengerwa. Aidha ameahidi zawadi nono kwa timu hiyo ikiwemo shilingi milioni 40 endapo watafuzu robo fainali, shilingi milioni 80 wakifuzu kucheza nusu fainali na shilingi milioni 100 waki...

Waziri Mchengerwa Ampongeza Bondia Kiduku kwa Kumkalisha M-Misri

Image
  Na John Mapepele. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa pongezi kwa   Bondia   Mtanzania Twaha Kiduku  kwa kumchapa kwa alama  za majaji wote watatu (unanimous decision)  Bondia  Abdo Khaled kutoka  Misri. Kwa ushindi huo, bondia Kiduku ameweza  kutetea  ubingwa wake wa  UBO Afrika (UBO all Africa Champion)  na Mkanda mpya wa ubingwa wa Mabara  (UBO Intercontinental). Hili ni pambano la 20 kushinda  kwa Kiduku , akitoka  sare 1 na kupoteza  8 akiwa na rekodi ya kucheza  mapambano 29. Mhe. Mchengerwa amefafanua kwamba dhamira ya Serikali  kwa sasa ni kutumia michezo kuitangaza Tanzania. Aidha, ametoa wito kwa wanamichezo kuthamini michezo na kufanya kama kazi inayoweza kubadili maisha yao na kuinua uchumi wa nchi kwa ujumla. Amesema, Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan itaendelea kusaidia wanamichezo w...

Hafla ya kuiaga Serengeti Girls, Mhe. Mchengerwa atoa maagizo mazito kwa Mkurugenzi mpya wa Michezo

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.  Mohamed Mchengerwa leo Septemba 21, 2022 amewaongoza watanzania kuiaga timu ya Serengeti Girls  kwenda Kombe la Dunia huku akitoa maelekezo mahususi kwa Kaimu Mkurugenzi mpya wa Michezo kuhusu kuendeleza sekta hiyo. Katika hafla ya kuiaga timu hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mhe. Mchengerwa amekabidhi BIMA na  vifaa mbalimbali  vya michezo ambapo pia Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi  na wadau mbalimbali wa michezo walishiriki. Mhe. Mchengerwa  amemtaka Kaimu Mkurugenzi mpya, Ally  Mayay kuleta maboresho kusudiwa kwenye Sekta ya Michezo na endapo hataweza ataondolewa. Mbali na hayo,  Mhe. Mchengerwa amempa  maelekezo  mahususi ambayo ametaka yafanyiwe kazi mara moja. Maelekezo hayo ni pamoja na kuweka mfumo wa Kutafuta vipaji vya wachezaji Kwa kushirikiana na Baraza la Michezo la Taifa ( BMT) na  Shirikisho la Soka nchini (TFF) pia kuandaa ...

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO

Image
   

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo yashirikiana na Wizara ya Maliasili kuitangaza Tanzania, kukuza utalii.

Image
  Na John Mapepele Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo na Wizara ya Maliasili na Utalii leo Septemba 16 na  taasisi wadau wa Wizara hizo kutoka  pande zote za Muungano wamekutana na kufanya kikao  kujadili  namna bora ya kutumia Utamaduni, Sanaa na Michezo kukuza utalii. Kauli hiyo ameitoa Waziri wa Utamaduni,  Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa baada ya kikao hicho cha pamoja ambapo amefafanua kuwa wizara yake imekuwa na matukio makubwa ambayo yanauhusiano mkubwa  na Utalii. Aidha, amesema kuna mambo ambayo wamekubaliana  kwa mshikamano na kutekeleza kwa pamoja  kuhakikisha kuwa sekta hizo zinakua. Amesisitiza kuwa  Kwa Ushirikiano baina ya  wizara itasaidia kupeleka taifa  mbele kwa kuwa sekta hizo zinategemeana. "Sisi katika Utamaduni tunao Utamaduni wa utalii, lakini katika michezo  kuna michezo na Utalii ambapo tunapokea wachezaji mbalimbali wa Kimataifa". Ameongeza  Mhe. Waziri Amesema tayari taifa limew...

MCHENGERWA AITAKA COSOTA KUTOA ELIMU YA KANUNI MPYA ZA ADA ZA VIBEBEA KAZI ZA SANAA NA MAKAMPUNI YA WASANII

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameitaka Taasisi ya Hakimiliki nchini (COSOTA)  kutoa elimu ya kutosha kwa wadau hususan wabunge      kuhusu mabadiliko makubwa yanayofanywa na taasisi hiyo ya kimuundo na kisekta ili kusaidia kuinua maisha ya wadau wa sekta ya Sanaa nchini. Waziri Mchengerwa ameyasema haya leo Septemba 14, mara baada ya kupitishwa  yeye na Naibu wake Mhe, Pauline Gekul na Menejimenti ya taasisi hiyo kwenye kikao cha kujadili  rasimu ya kanuni ya uanzishwaji wa Ada kwa vibebea kazi za ubunifu (blank device) na uanzishwaji wa makampuni binafsi ya   wasanii ya ukusanyaji na ugawaji mirahaba (CMO). Amewataka kuharakisha mchakato wa kukamilisha rasimu hizo ili  zisainiwe  na kuanza kutumika mara moja hatimaye wasani na wadau mbalimbali wa kazi za Sanaa waweze kunufaika na kazi zao. "Harakisheni, ninakwenda kuisaini kanuni hizi mara moja ili wasanii  wafaidi matunda ya...

Mhe. Mchengerwa- Serikali kuendelea kuwekeza kwenye timu zinazofanya vizuri, Gofu Wanawake, Twiga stars wanga'ra

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema  Serikali itaendelea kuwekeza kwenye timu zinazofanya vizuri huku akiwataka Watendaji wa michezo kufanya tathmini kwa zisizofanya  vizuri ili Serikali ichukue maamuzi magumu. Mhe. Mchengerwa ameyasema haya usiku wa leo hafla ya utoaji wa tuzo kwa washindi wa mashindano  ya Afrika ya Gofu ya Wanawake -All Africa Competition Trophy (AACT) yaliyofanyika kuanzia  Septemba, 6-8, 2022 kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam na kushirisha nchi 20. Katika mashindano hayo Tanzania imeshika nafasi ya tatu wakati Morocco imeshika nafasi ya pili na nchi ya  Afrika Kusini kuwa mshindi wa kwanza. Ameipongeza timu ya Tanzania kwa kushika  nafasi ya tatu huku akifafanua kuwa  hayo ni matunda ya uwekezaji mkubwa wa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye michezo katika kipindi kifupi cha uongozi wake. Aidha, ameipongeza timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Twiga Stars kwa ku...

Serikali kuzindua mikopo isiyo na riba kwa wasanii - Mhe. Mchengerwa

Image
  Na John Mapepele Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo inakwenda kufanya uzinduzi wa utoaji wa mikopo kupitia Mfuko wa Utamaduni  ndani ya siku kumi kutoka sasa ili wasanii waweze kunufaika na mfuko huo ambao Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeuanzisha kuwanufaisha wasanii. Hayo yamesemwa  leo Septemba 7, 2022 na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa baada ya kikao na Watendaji wa Benki ya CRDB, Benki ambayo itatumika kwa ajili kutoa mikopo hiyo kwa niaba ya Serikali. Mhe. Mchengerwa amesema  uzinduzi huo utafanywa  ndani ya siku kumi kuanzia sasa ambapo amefafanua kuwa mikopo hiyo haitakuwa na riba yoyote ili wasanii wengi waweze kunufaika mikopo hiyo. Amesema  katika  tukio la uzinduzi wa mikopo hiyo  pia  Muongozo wa Uendeshaji  Mfuko utazinduliwa  ili vigezo na masharti ya uombaji wa mikopo vieleweke kwa  waombaji. Aidha,  amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya...